Smile FM Radio
Smile FM Radio
September 2, 2025, 3:28 pm

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya aprili mpaka juni 2025, Takukuru inahakikisha kuwa fedha zote za maendeleo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa
Na Kudrat Massaga
Katika kipindi cha mwezi April hadi June, Takukuru Mkoa wa Manyara imefanikiwa kurejesha jumla ya madawati 20 yaliyofanyiwa ubadhirifu.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari inabainisha kuwa Hiyo ni kutokana na ufuatiliaji uliofanyika ilionyesha kuwa mzabuni alilipwa sh 5 million mnamo tarehe 19 June 2024 kwa ajili ya matengenezo ya madawati 50 ya shule yamsingi Oltepeleki iliyopo katika Kijiji cha loiborsiret wilaya ya simanjiro.
Taarifa hiyo inabainisha kuwa mzabuni aliwasilisha madawati 30 pekee na fedha zilizokusudiwa kwa ajili ya kutengeneza madawati mengine 20 yenye thamani ya shs 2 milion zilifanyiwa ubadhirifu na mtendaji wa kijiji kwakushirikiana na mzabuni.
Mbali na hilo Takukuru Mkoa wa Manyara imefuatilia jumla ya miradi ya maendeleo saba yenye thamani ya shs 14.7 billion inayohusu sekta za elimu, Afya na miundombinu ya barabara na maji.
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, Takukuru imetoa wito kwa wananchi wote kuepuka kushiriki katika vitendo vya rushwa na kuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za kukomesha na kutoa taarifa pale wanapoona kuwepo kwa dalili za rushwa.