Smile FM Radio

Kinnapa na mpango wa kuwarudisha watoto wakike shuleni

July 4, 2025, 3:40 pm

Picha ya mkurugenzi wa KINNAPA Abraham Akilimali, akizungumza na waandidhi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo

Wito umetolewa kwa waandishi wa habari Babati Mkoani Manyara kuendelea kuhamasisha sera ya haki ya kuwarudisha watoto wa kike shuleni.

Na Linda Moseka

Mkurugenzi wa shirika la KINNAPA Abraham Akilimali ametoa rai kwa waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kuendela kuzungumzia na kuhamasisha sera ya haki ya kuwarudisha watoto wa kike shuleni.

Amezungumza hayo mbele ya waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Babati Manyara na kusema kuwa ipo kazi kubwa ya kuzungumzia sera hiyo kwa kuwa tayari serikali imesharuhusu basi ni vyema kuelewesha wazazi na jamii ili watoto hao waweze kupata haki zao.

Sauti ya Mkurugenzi wa KINNAPA

Paulina Ngurumwa ambae ni afisa maendeleo shirika la KINNAPA. amesema elimu ni haki kwa watoto wakike na nimaendeleo endelevu hivyo mtoto wakike apewe nafasi kwa kuwa mpaka sasa kupitia mfuko wa kuwasaidia watoto wa kike waliokatiza masomo wameweza kuwasaidia kupata cherehani tano ambayo ilikua ni kama mtaji wa wao kupata miradi ya kuwawezesha kiuchumi ambao mpaka sasa wameweza kujishonea sare zao.

Sauti ya Paulina Ngurumwa

Nae afisa maendeleo ya jamii mkuu Lilian Bujune ametoa pongezi kwa shirika la kinnapa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuanzisha mabaraza,club za watoto kwakuwa ndiyo azimio lililobebwa na waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maluum.
Amesema asilimia 60 ya vitendo vya ukatili vinafanyika nyumbani hivyo mtoto anapokuwa na fursa ya kujieleza shuleni inakuwa raisi walimu kumsaidia kwa kupata matibabu na kuchukua hatua.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii mkuu Lilian Bujune

Kwa mujibu wa afisa maendeleo ya Jamii Babati DC Mathias Focus amesema Halmashari imeonyesha mafanikio katika kupambana na ukatili na hiyo nikwamujibu wa takwimu na hali ilivyo ikiwa mwaka 2022 kulikuwa na visa vya ukatili 330 vya ukatili wa namna mbali mbali ,kufikia mwishoni mwa mwaka 2024 viliripotiwa visa 293 na kwa kipindi cha january mpa june mwaka huu 2025 kuna kesi 56 za ukatili zilizoripotiwa polisi na katika hizo kesi 50 zimefikishwa mahakamani ambazo zipo katika hatua mbalimbali kwahivyo hiyo ni hatua ya kujivunia.

Sauti ya Afisa maendeleo ya Jamii Babati DC Mathias Focus
Hata hivyo Afisa elimu taaluma babati DC Judith Fransis Materu ameeleza kuwa wanafunzi wana fursa ya kurejea shuleni baada ya kuacha masomo kwa changamoto mbalimbali hivyo kwa babati wanafunzi waliorejea shuleni kwa mwaka 2023/2024 na mpaka sasa 2025 baada kuacha masomo wamefikia 21 na kati ya hao wasichana wako 10 na wavulana 11.

Vilevile amempongeza rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mh,Samia Suluh Hasan kwa kuwaruhusu watu wa mashirika mbalimbali kama Kinnapa kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu ambayo ni bora kwa malengo ya kufikia ndoto za maisha yao ya baadae.