Smile FM Radio

‘Ufugaji wa nyuki una faida’

May 21, 2025, 2:23 pm

Picha ya Afisa ufugaji wa nyuki Halmashauri ya wilaya ya Babati, Fabian Mandas

Imeelezwa kuwa ufugaji wa nyuki ni muhimu katika mazingira yetu na kwa binadamu kwa ujumla kwani ni chanzo cha tiba pia.

Na Kudrat Massaga

Jamii imetakiwa kujifunza namna ya kufuga nyuki badala ya kuwaharibu kwani mazao yake yana thamani kubwa katika maisha ya binadamu na jamii kwa ujumla.
Hayo yamezungumzwa na Afisa ufugaji wa nyuki Halmashauri ya wilaya ya Babati Fabian Mandas wakati akizungumza na Smile Fm Radio.
Mandas amesema kuwa licha ya faida moja inayojulikana na watu walio wengi kutoka kwa nyuki bali pia mdudu huyo ni chanzo cha utunzaji wa mazingira.

Sauti ya afisa ufugaji wa nyuki fabian Mandas

Akumuelezea mdudu nyuki Mandas amesema manufaa yake ni mengi kuliko madhara hivyo ni vema jamii kujua umuhimu wake ili kuweza kunufaika nayo.

Sauti ya afisa ufugaji wa nyuki fabian Mandas
Hata hivyo mtaalam huyo wa nyuki alitoa elimu ni namna gani ya kujikinga na nyuki hasa pale wanapomvamia binadamu ili wasiweze kuleta madhara makubwa.

Siku ya nyuki Duniani huazimishwa kila tarehe 20 mei kila mwaka, na kwa Tanzania maadhimisho hayo yalifanyika Jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na yalikwa na kauli mbiu isemayo” Nyuki ni muhimu kwa uhai na uchumi, tuwahifadhi.