Smile FM Radio
Smile FM Radio
May 19, 2025, 11:38 am

Picha ya Afisa uchaguzi Bashan Kinyunyu
Wananchi wametakiwa kujitokeza kwenye kuboresha taarifa pamoja na kujiandikisha kwa wale waliokosa nafasi hiyo awamu ya kwanza
Na Kudrat Massaga
Wananchi wamesisitizwa kijitokeza kwa wingi kwenye vituo vilivyotangazwa kwajili ya kuboresha taarifa zao pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa kila mwenye sifa ili waweze kutimiza haki ya kikatiba ya kupiga kura.
Wito huo umetolewa na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Babati mjini Bashan Kinyunyu wakati akifanya mahojiano na smile fm Radio.
Kinyunyu amesema ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hii ambayo ni kwa awamu ya pili kwa wale ambao hawakuweza kujiandikisha na kuboresha taarifa katika daftari la kudumu kufanya hivyo sababu ni takwa la kikatiba.
sauti ya afisa uchaguzi Bashan Kinyunyu
Kwa upande mwingine pia kinyunyu amesema zoezi hili pia limeambatana na zoezi la uwekaji wazi daftari la awali la mpiga kura ambapo amesema kila mwananchi aliyejiandikisha awamu ya kwanza anawajibika kwenda kuangalia usahihi wa majina yake pamoja na kuangalia kama kuna majina ambayo sio ya sehemu husika au kama wapo waliofariki dunia waweze kutoa taarifa ili watolewe kwenye daftari la kudumu.
sauti ya afisa uchaguzi Bashan Kinyunyu
Zoezi hili la uboreshaji ni la awamu ya pili likiwa linajumuisha mikoa 16 na Mnyara ikiwemo na limeanza tarehe 16 mei 2025 na litatamatika tarehe 22 mei 2025.