Smile FM Radio

DC Kaganda arejesha amani kirudiki

May 1, 2025, 8:58 am

Mkuu wa wilaya ya Babati Mh Emmanuela Kaganda akizungumza na kutatua changamoto za wananchi wa kirudiki.

Na Salum Majey

Wananchi wa Kiru Diki, Wilaya ya Babati, wameonyesha furaha na shukrani zao kwa Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda kwa juhudi zake zilizofanikisha kurejeshwa kwa amani katika eneo lao baada ya miaka kadhaa ya migogoro na mvutano kati yao na wawekezaji.

Hali hiyo ilidhihirika wazi katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kiru Diki, uliofanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Wananchi hao walibubujikwa na maneno ya furaha, wakikiri hadharani kuwa sasa wanaishi kwa amani na utulivu mkubwa.

Picha ya wakazi wa kirudiki
Sauti za wananchi wa kirudiki kwa mkuu wa wilaya ya Babati mji

Kwa miaka mingi Kiru Diki imekuwa ikikumbwa na migogoro ya ardhi iliyosababisha sintofahamu na ukosefu wa amani. Hata hivyo, baada ya Mkuu wa Wilaya kuingilia kati, kusimama kidete kutafuta haki, na kufanya ziara za mara kwa mara kwa ajili ya kutoa elimu na kujenga uelewa kwa wananchi, hali imebadilika na eneo hilo sasa linashuhudia utulivu wa kipekee.

Katika mkutano huo, Mhe. Kaganda alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, mshikamano na maendeleo kwa ajili ya kujenga Kiru mpya iliyo imara na yenye matumaini mapya. Aidha, kama sehemu ya kuhamasisha mshikamano kwa vijana, alikabidhi mipira mitano na seti ya jezi kwa ajili ya kuimarisha timu zao za michezo, akibainisha kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kukuza amani na mshikamano katika jamii.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda akizungumza na Wananchi wa kirudiki.

Kwa sasa, wananchi wa Kiru Diki wanaendelea kujenga maisha yao kwa matumaini mapya, wakiamini kuwa kwa mshikamano na uongozi bora na maendeleo.