Smile FM Radio
Smile FM Radio
April 30, 2025, 12:41 pm

Picha ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Babati Stephano Yodal akiwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Babati mjini Cesilia mbangati.
Na kudrat Massaga
Vikundi vinavyohusika na ukopeshaji pamoja na wakopaji kwenye vikundi vya mtaani wametakiwa kuzijua sheria ili kuepusha migogoro itakayopelekea kuvunja sheria kwenye kudai au kudaiwa.
Hayo yamezungumzwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Stephano Yodal wakati akifanya mahojiano na Smile Fm katika kipindi cha Tubonge .
Kwa upande wake Cecilia Mbangati ambae ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya mwanzo Babati mjini amesema ni muhimu inapotokea watu kukopeshana kuwe na ushahidi wa maandishi pamoja na mtu mwingine wa tatu ili kupatikana haki ya anayedai pale inapotokea changamoto kwenye kulipwa.
Hata hivyo Bi Cecilia amesema upo umuhimu wa usuluhisho kwenye kumaliza mashauri ya madai kwani hupelekea watu kuishi kwa upendo na amani kuliko kufikisha kesi mahakamani.
Sauti ya Hakimu Cecilia Mbangati
Sauti ya Hakimu Cecilia Mbangati