Smile FM Radio

Waadhimisha miaka 61 ya muungano wilayani Babati

April 29, 2025, 12:56 pm

Mkuu wa wilaya ya Babati Mhe Emanuela Kaganda akishiriki zoezi la usafi mjini Babati kwenye maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanzania.

“Tanzania imeweza kusimamia Muungano kwa sababu waasisi wa hawakuwa na maslahi binafsi bali walikuwa na mapenzi mema na nchi

Na Kudrat Massaga

Wananchi Mkoani Manyara wametakiwa kuwashukuru viongozi wote waliopita na waliopo sasa madarakani kwa kuendelea kuenzi na kudumisha Muungano wa Tanzania

hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati mjini Mh Imanuela Kaganda wakati wa sherehe za maadhimisho ya Muungano wa miaka 61 ya Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 April 2025, ambapo ametumia siku hiyo kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Amesema Tanzania imeweza kusimamia muungano kwa sababu waasisi wa hawakuwa na maslahi binafsi bali walikuwa na mapenzi mema na nchi zao ili kuweza kutengeneza nchi moja ambayo imeungana na imekuwa imara kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Babati Mhe Emanuela Kaganda

Sambamba na hilo Kaganda ameahidi kuwa wataendelea kuwahudumia wananchi kwa upendo, weledi na huruma zaidi ili kila mmoja aweze kusimama kwenye nafasi yake ili kujenga Tanzania ambayo ni imara yenye mshikamano na yenye watu ambao wana mafanikio na maendeleo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA Mkoa wa manyara Zainab Rajab amesema anaunga mkono juhudi za serikali katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani wameona kuna manufaa mengi hasa ya kiuchumi na kibiashara.

Sauti ya Katibu Mtendaji wa chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA Mkoa wa manyara Zainab Rajab

Maadhimisho hayo katika wilaya ya Babati yalihusisha Taasisi, Kamati ya Usalama, watumishi wa Halmashauri, viongozi wa mitaa pamoja na wananchi mbalimbali.