Sauti ya Amani

Amani ni msingi wa maisha ya kila siku katika familia, jamii na taifa kwa ujumla. Mara nyingi watu huiona amani kuwa ni hali ya kutokuwepo kwa vita au vurugu, lakini ukweli ni kwamba amani huanzia katika maneno yetu, matendo yetu na namna tunavyowatendea wengine.

Penye kuheshimiana, kusikilizana na kuvumiliana, ndipo amani ya kweli hujengwa. Migogoro mingi katika jamii huanza kwa maneno yasiyo ya kweli, uvumi na hasira zisizodhibitiwa. Watu wanaposhindwa kuthibitisha ukweli au wanaporuhusu chuki kutawala mioyo yao, mahusiano mazuri huvunjika na maelewano hupotea. Ndiyo maana kila mmoja ana jukumu la kuwa sehemu ya suluhisho badala ya kuwa chanzo cha migogoro. Thamani ya amani huonekana zaidi pale inapopotea.


Amani ni hazina kubwa ambayo haiwezi kununuliwa kwa fedha. Tuilinde kwa uvumilivu, upendo na kuheshimiana ili vizazi vya sasa na vijavyo viendelee kuishi katika mazingira yenye utulivu na matumaini.

Sauti ya Amani Epsode 1
Sauti ya Amani Epsode 2
Sauti ya Amani Epsode 3
Sauti ya Amani Epsode 4
Sauti ya Amani Epsode 5
Sauti ya Amani Epsode 6
Sauti ya Amani Epsode 7
Sauti ya Amani Epsode 8
Sauti ya Amani Epsode 9
Sauti ya Amani Epsode 10
Sauti ya Amani Epsode 11
Sauti ya Amani Epsode 12

Tuitunze amani yetu, amani inaanza na mimi

Ujumbe huu umeletwa kwenye na mtandao wa redio za kijamii nchini – TADIO