Kagera Community Radio

Mgambo watakiwa kuzuia magendo na wahamiaji haramu

August 28, 2025, 11:42 pm

Askari mgambo waliohitimu mafunzo wilaya ya Karagwe

Askari wa jeshi la akiba (mgambo) mkoani Kagera wametakiwa kuwa malinzi wa raia na mali zao na kuwa wazalendo katika kulilinda taifa lao dhidi ya vitendo vya uhalifu.

Na Anold Deogratias

Mkuu wa wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Erasto Yohana Siima amewataka askari wa jeshi la akiba mgambo kuzuia magendo yanaingia au kutoka nchini na kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini hali inayoweza kuhatarisha  usalama wa nchi.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa vitendo ya Askari hao yaliyofanyika katika shule ya msingi Nyakato wilayani Bukoba, Dc, Siima amewataka kutumia ujuzi waliopata katika mafunzo hayo kuhakikisha wanathibiti vitendo vya kihalifu ikiwemo magendo na wahamiaji haramu.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka askari mgambo hao kutotumia mafunzo waliyoyapata kuwanyanyasa wananchi bali yawe na faida katika kuwalinda raia na mali zao pamoja na taifa kwa ujumla.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Yohana Siima

Kwa upande mwingine akifunga mafunzo ya mgambo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laizer, mkuu wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagaera Kanali mstaafu Hamis Maiga, amewataka askari hao kuwa na nidhamu wakati wa utekelezaji wa majuku yao pamoja na kuwa wazalendo kwa taifa lao.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagaera Kanali mstaafu Hamis Maiga

Mkuu wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagaera Kanali mstaafu Hamis Maiga

Awali wakiwasilisha risala yao askari hao wa akiba wameomba kupunguziwa gharama za sare zao pamoja na kuomba kujumuishwa na kupewa kipaumbele katika kazi za ulinzi katika jamiii.

Askari mgambo waliohitimu mafunzo

Mafunzo hayo yalianza tangumwezi April na kutamatika mwezi Agost mwaka huu.