Kagera Community Radio

Shilingi bilioni 45 kujenga madaraja matano Kagera

August 21, 2025, 2:07 am

Ujenzi wa daraja la Kanoni manispaa ya Bukoba

Shilingi bilioni 45 zinatarajiwa kutumika kujenga madaraja matano mkoani Kagera ambayo yamekuwa hatarishi hasa nyakati za mvua hali inayokwamisha shughuli za usafiri na ufarishaji mkoani Kagera.

Na Avitus Kyaruzi

Serikali inatekeleza ujenzi wa madaraja matano ambayo yamekuwa hatarishi hasa nyakati za mvua mkoani Kagera, ujenzi unaoghalimu shilingi bilioni 45.

Akielezea maendeleo ya miradi hiyo Meneja wa wakala wa barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Kagera Mhandisi Ntuli Mwaikokyesa amesema kuwa miradi hiyo imefikia hatua tofauti za utekelezaji na kuongeza kuwa kwa kasi ya wakandarasi miradi hiyo itakamilika kwa muda uliopangwa kwa mujibu wa mikataba.

Mhandisi wa TANROAD, Kagera Ntuli Mwaikokyesa

Aidha Mhandisi Ntuli ameongeza kuwa Daraja la Kanoni linajengwa na mkandarasi Abemulo Consultant lililopo mjini kati ambalo lina urefu wa mita 30 na Barabara za maungio mita 600 limefikia asilimia 50 na kukamilika kwakwe kutarahisisha usafishaji na kupendezesha mji wa Bukoba.

Sauti ya meneja wa TANROADS mkoa wa Kagera Mhandisi Ntuli Mwaikokyesa
Kwa upande wake mwakilishi wa mkandarasi Abemulo mhandisi Aloyce Anatory Kamala amesema kuwa mradi huo utakamilika kwa muda kwa kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana huku akieleza kuwa kukamilika kwa Daraja hilo kutaondoa tatizo la mafuriko katika eneo hilo.

Sauti ya Mhandisi Aloyce Anatory Kamala
Pia sambamba na ujenzi wa Daraja la Kanoni mkandarasi Abemulo anatekeleza mradi wa Barabara ya njia nne ambao umefikia asilimia 40 ya utekelezaji wake kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 5.

Ujenzi wa daraja la Kanoni ukiendelea
Ujenzi wa daraja la Mishango wilayani Muleba ukiendelea