Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
August 17, 2025, 1:44 am

Viongozi na wananchi katika jamii wameaswa kutanguliza na kutenda haki kwanza ili kuweza kupata Amani na kuleta utulivu katika jamii hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Na Anold Deogratias
Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage amesisitiza viongozi na wananchi hapa nchini kuimiza haki na Amani ili nchi iwe na utulivu hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mhashamu, Baba Askofu Mwijage, amesema hayo wakati wa homilia yake katika adhimisho la Misa takatifu, katika Kigango cha Mtakatifu Yohane Mtume- Ihunga, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima- Rukindo Jimbo Katoliki Bukoba.

Amesema hakuna Amani bila haki hivyo amewasisitiza vingozi kutanguliza haki kwanza, na kusisitiza msingi wa Amani ni haki.
Sauti ya Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage
Aidha amewataka wazazi na walezi kutunza uzao, kuwafundisha watoto wao sala na imani na kuwaandaa watoto wao katika kuitetea imani na kuliombea taifa la Tanzania amani.
Sauti ya Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage
Pia Askofu Mwijage amesema kuwa, kila familia inayo wajibu wa kulinda imani Katoliki na kamwe wasikubali kudanganyika na madhehebu yanayo chipukia, na kuwasihi wazazi kulinda kanisa lao na vizazi vijavyo kwa gharama yoyote kwa kuwa na Imani thabiti na kuilinda kupitia matendo mema.