Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
July 11, 2025, 11:30 pm

Wanunuzi wa vyuma chakavu na mafundi bomba mkoani Kagera wametakiwa kutoa ushirikiano na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bukoba (BUWASA) ili kuwabaini watu wanaoiba na kuharibu miundombinu ya maji.
Na.Avitus Kyaruzi
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bukoba (BUWASA) imewataka wanunuzi wa vyuma chakavu na mafundi bomba kutoa ushirikiano na mamlaka hiyo katika kuwabaini watu wanaoiba na kuharibu miundombinu ya maji.
Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau wa maji na wanunuzi wa vyuma chakavu, katika ofisi za mamlaka hiyo manispaa ya Bukoba, mkurugenzi wa BUWASA, John Silati amesema wizi wa mita za maji na bomba za maji za mamlaka hiyo umekuwa ukipelekea hasara kubwa kwa mamlaka na kwamba atakayebainika hatachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo faini au kifungo gerezani.
Sauti ya mkurugenzi wa BUWASA, John Silati

Naye mkurugenzi huduma kwa wateja wa BUWASA, Bw.Deogratias Sense amewatahadharisha wananchi wanaoiba maji kwa kuchepusha bila kupitia kwenye mita, ambapo amewataka mafundi bomba kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria endapo watawabaini.
Sauti ya mkurugenzi huduma kwa wateja wa BUWASA, Bw.Deogratias Sense
Nao baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho Omary Mzamiru, Kamugisha Medard na Yazid Yassin Almas waneitaka mamlaka hiyo kuwadhibiti baadhi ya wafanyakazi wao wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiuza vifaa vya mamlaka hiyo bila kufuata utaratibu.
sauti ya wanunuzi wa vyuma chakavu na mafundi bomba
