Kagera Community Radio

Wabaeba mizigo bandari ya Bukoba walipwa fedha zao

June 29, 2025, 10:16 am

Wabeba mizigo katika bandari ya Bukoba wakiendelea na shughuli zao

Kampuni ya IFS imetekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjati Fatma Mwassa la kuwalipa fedha zaidi ya shilingi milioni 20 wabeba mizigo katika bandari ya Bukoba, walizokuwa wanadai kwa kipindindi cha miezi miwili.

Mmoja ya wabeba mizigo bandari ya Bukoba akisaini ili kulipwa fedha yake

Na Anold Deogratias

Wabeba mizigo katika bandari ya Kastam (makuli) iliyopo manispaa ya bukoba mkoani Kagera wamelipwa fedha zo walizokuwa wanaidai kampuni ya IFS, zaidi ya shilingi milioni 20 baada ya kufanya kazi kwa wiki sita bila kulipwa.

Wakizungumza mara baada ya kupokea fedha hizo wa baadhi ya wabeba mizigo hao Phinias Elias na Mohamed Oziri, wameshukuru kulipwa fedha zao na kutaka kuheshimiwa kwa makubaliano walioingia na mzabuni mpya kampuni ya IFS ya kulipwa fedha zao kila wiki.

Sauti wabeba mizigo bandari ya Bukoba

Kwa upande wake msimamizi wa kazi za kila siku kutoka kampuni ya IFS bandari ya Bukoba Godfrey Bwana amesema kuwa wabebea mizigo hao wamemaliza fedha zao zote na kuahidi kutojitokeza tena kwa hali hiyo ya kudaiwa kwa muda murefu.

sauti ya Godfrey Bwana msimamizi wa kazi za kila siku kutoka kampuni ya IFS

Kulipwa kwa fedha hizo ni kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Kagera hajjat Fatma Mwassa, baada ya kufika katika bandari hiyo na kusikiliza kero za za wabeba mizigo hao na kutaka kulipwa fedha zao nadani ya siku tatu baada ya kugoma kushinikiza kulipwa fedha zao za miezi miwili.

Sauti mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjati Fatma Mwassa

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Kagera ameitaka mamlaka ya usimamizi wa bandari TPA kuangalia upya ufanisi wa kampuni ya IFS, kwani imeshindwa kutimiza makubaliano ndani ya muda mfupi hivyo kutia mashaka kama wanauwezo wa kuendesha shughuli za upakiaji na ushushaji wa mizigo bandarini.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa