Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
February 5, 2026, 10:14 pm

Fainali iliyoandaliwa na Diwani wa Butiama imetamatika leo kwa tim ya Bodaboda kushinda ubingwa huo kwa kuwafunga timu ya Mwenge kwa goli moja kwa sifuri.
Na Oscar Mwakipesile
Timu tishio kwasasa Wilayani Butiama Mkoani Mara bodaboda fc imekuwa mabingwa mara mbili mfululizo katika ligi mbili tofauti na kujishindia kombe pamoja na pesa taslimu pamoja na mpira na jezi kama zawadi ya mshindi huku mshindi wa pili ikipewa zawadi ya jezi zenye thamani ya shiling laki tatu ,Big cup ni ligi iliyoandaliwa na Diwani wa Butiama kwa lengo la kuunda timu ya kata itakayoshiriki mashindano ya Wilaya yaliyoandaliwa na Mbunge wa Butiama Mh.Mahela yatakayoanza tarehe 8 mwezi huu katika viwanja vya mwenge.

Pamoja na kumalizika kwa mchezo wa fainali pia ilitangazwa timu iliyoundwa kutokana na michuano hiyo itakayoshiriki mashindano ya wilaya ya Butiama yatakayoanza jumapili kwenye viwanjka vya mwenge hapa Butiama.
