Butiama FM Radio

RC Mara aongoza kusanyiko la ushirikishwaji wa jamii

October 3, 2025, 9:56 pm

Mkuu wa mkoa wa Mara Mh. Kanali Evans Mtambi akikata utepe wa Butiama fm.

Kusanyiko la ushirikishwaji wa jamii na uhamasishaji wa haki ya juu, kuweka mkakati wa mawasiliano mazuri kuitangaza Butiama FM Radio 93.1.

Na Swaiba Oscar

Mkuu wa mkoa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye kusanyiko hilo aliongoza na kuwasihi wananchi wa butiama kutoa ushirikiano kwa radio jamii Butiama fm ili kuleta maendeleo katika wilaya nzima ya Butiama pia aliwasihi maafisa usafirishaji maarufu kama boda boda kutoa ushirikiano kwenye uhamasishaji na kuleta ushiriki zaidi kuleta maendeleo katika jamii kupitia radio butiama fm 91.3.

Baadhi ya wakazi wa Butiama wakifurahia kusanyiko hilo mbele ya mkuu wa mkoa.
Mkuu wa mkoa akiwa na Chifu wa wazanaki wakiteta jambo kwenye kusanyiko la uhamasishaji na ushirikishwaji wa jamii lililoandaliwa na Butiama fm 91.3

Kusanyiko hilo lilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo

Nd. Aziza Baruti – Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama

Col. Evans Mtambi -Mkuu wa Mkoa wa Mara

Mhe. Thecla Mkuchika – Mkuu wa Wilaya ya Butiama

Chief Japhet Wanzagi na

Dk. Wilson Mahera – Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Butiama