Butiama FM Radio

Utafiti juu ya kuzipa heshima kazi za wabunifu

April 23, 2025, 2:58 pm

Ayeta Anne Wangusa Mkurugenzi wa Cdea na mtafti kutoka ILO.

Shirika la Kazi Duniani ILO kwa kushikiana na UNESCO wamefanya utafti ni kwa namna gani wanaweza kuzipa heshima kazi za wabunifu kulingana na hadhi ya kazi hiyo.

na Swaiba Oscar

Akizungumza alipokuwa akifanyiwa mahojiano mkurugenzi wa culture development east Africa cdea Ayeta anne wangusa akiwa mmoja ya walio husika kwenye utafti huo na wengine kutoka nchi zingineamesema .

‘’Tumefanya utafti katika nchi nne zikiwemo Tanzania ,Nigeria ,Congo DR na Africa Kusin ambapo kila nchi tulikuwa tunaangalia ubunifu wa aina tofauti Tanzania tulijikita kwa wabunifu wa mavazi na viwanda vidogodogo

Vya nguo huku Nigeria waliangalia upande mzima wa film ambapo walijikita zaidi pale Nollywood huku Sauth Africa wao walifanya upande wa muziki Zaidi na Congo DR waliangalia upande mzima wa wananguaji wa  kwenye mziki hivyo kupelekea utafti kufanyika katika nchi nne za Africa”.

Lakini kote huko ushirkiano ulikuwa mdoho sana  hivyo kulazimika kutumia tafti zilizowahi kufanyika hapo nyuma na tukagundua sera na sharia bado hazikovizuri kwa ajili ya kutambua wabunifu na haki zao ili ziweze kupatiwa hesima na ni vyema tukaanza na marekebisho yay a sera na sharia za nchi kwanza kuwatambua wabunifu.alimaliza Ayeta wangusa.

Ayeta wangusa akiwa anafanya mahojiano kupitia radio yetu.