Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
April 23, 2025, 10:27 am

Kijana Juma Mwita Sagwe afunga goli pekee dhidi ya Zambia kwenye mchezo wa AFCON 2025 Morocco.
Na Kelvin Ayoub
Juma Mwita Sagwe ambaye ni zao la Brazuka Sports Promotion Ltd ambao walifanya mashindano ya kuibua vipaji vya vijana mwaka 2023 na kufanikiwa kuchagulia kuingia kwenye programu hiyo. Programu hiyo iliyofanyika mikoa 8 Tanzania bara na visiwani ilihusisha vijana zaidi ya 200.
Baada ya kunolewa ndani ya Brazuka Sports Promotion Ltd, alichaguliwa kuingia kwenye timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wa chini ya miaka 17.
Kwa mara kwanza kwenye TotalEnergies CAF Under-17 Africa Cup of Nations (AFCON), Zambia ilikutana uso kwa uso na Tanzania tarehe 31 mwezi 3 ambapo Zambia iliibuka na ushindi wa goli 4-1 ikiwa goli pekee la Tanzania lilifungwa na mchezani Juma Mwita Sagwe katika dakika ya 95.
