Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
February 12, 2026, 8:14 pm

‘Tunapaswa kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa wanaenda shule madiwani waote na wakuu wa idara ya elimu mkasimamie hilo na kuzingatia chakula kinapatikana shuleni Kwa ajili ya lishe Kwa wanafunzi” Katibu tawala Wilaya ya Bunda Salmu Alfan Mtelela
Na Amos Marwa
Serikali Wilaya ya Bunda imewataka madiwani Kwa kushirikiana na wananchi wote kuhakikisha wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni waweze kuripoti ili Kwendelea na masomo yao.
Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Wilaya ya Bunda, Salmu Alfan Mtelela aliemwakilisha mkuu wa Wilaya wakati wa salamu za serikali katika kikao Cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda na kusema kuwa darasa la awali ni Asilimia 92, darasa la kwanza asimilia 92, na sekondari ni asimilia 94
Katika hatua nyingine Mtelela amesema wananchi Wilaya ya Bunda wanapaswa kutumia fursa ya bima ya afya Kwa wote ambayo imetangazwa na serikali kuu ili kupunguza gharama za matibabu Kwa watu wasio na uwezo wa kiuchumi.

Baraza hilo la madiwani limejadili na kuazimia masuala mbalimbali ikiwemo Malipo ya fidia ya wananchi walioharibiwa mazoa yao na wanyama , kupokea iaarifa ya utekerezaji wa miradi ya maji kutoka Mamlaka za maji mjini na vijijini, utekerezaji wa miradi ya Barabara , uwekezaji katika mlima Kaswaka na Ukusanyaji wa mapato Kwa ajili ya maendeleo halmashauri ya mji Bunda.
