Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
October 20, 2025, 9:30 pm

”Hakuna jasho la Mtu linalotumika bure kama wananchi watachagua viongozi wanaotoa rushwa viongozi hao watakaposhinda watatumia muda wao mwingi kurejesha fedha walizotumia kuhonga wananchi hivyo huduma za kijamii kuwa duni”William Eliyau ambae ni Mchunguzi kutoka tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)
Na Amos Marwa
Wananchi mkoa wa Mara wameaswa kujiepusha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu ili kuchagua viongozi waadilifu na watakao waletea maendeleo.
Hayo yamebainishwa na William Eliyau ambae ni Mchunguzi kutoka tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari na kusema kuwa wananchi wanapaswa kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuongeza kuwa madhara ya rushwa yanaweza kusababisha kupata viongozi wasio leta maendeleo katika jamii.