Bunda FM Radio

Wanafunzi Bunda wahamasishwa kupanda miti

June 14, 2025, 10:11 am

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Salama A wakijifunza kwa vitendo namna bora ya kuandaa kitalu cha miti. Picha na Revocatus Andrew

Upandaji miti ni njia mojawapo ya utunzaji wa mazingira,kupata kivuri na upatikanaji wa matunda ya kutosha katika jamii yetu Tegemeo Masiti mhifadhi misitu Wilaya ya Bunda.

Na Witness Joseph

Akizungumza na Bunda Fm Radio kwenye kipindi cha ukurasa mpya mhifadhi misitu(TFS) Wilaya ya Bunda bwana Tegemeo Masiti amesema wanafunzi ni vijana na nguvu kazi ya Taifa ivyo wana muda mzuri wa kufanya kazi iyo ya upandaji miti kwa sababu hawana majukumu mengine kwenye jamii zaidi ya kusoma.