Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
May 28, 2025, 1:26 pm

“tumekuwa tukiifunga barabara hiyo isitumike kwa ajili ya usalama wa watumiaji kwa kuweka kamba na mawe lakini watumiaji hao wamekuwa wakiifungua na kupita na ivyo kuhatarisha usalama wao,” meneja wa TARURA wilaya ya Bunda Injinia Ahimidiwe Kiluswa.
Na Amos Marwa.
Wakazi wa Mtaa wa Kilimani Halmashauri ya wilaya ya Bunda wameomba Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), kutengeneza daraja la barabara ya kilimani karibu na stendi mpya liloharibika kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Wakizungumza na Bunda FM Radio watumiaji wa barabara hiyo wakiwemo maafisa usafirishaji (BODA BODA) na watembea kwa miguu wamesema kutoboka kwa sehemu ya daraja hilo kumesababisha adha kubwa na kunaweza kusababisha ajali muda wowote.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Bunda Mji Injinia Ahimidiwe Kiluswa amedhibitisha kuharibika kwa daraja hilo na kusema kuwa tahadhari zinaendelea kuchukuliwa na mamlaka na kuongeze kuwa daraja hilo lipo kwenye mpango wa kutengezwa mwishoni mwa mwaka huu.
Barabara mbalimbali za mji wa Bunda zimekuwa zikiharibika mara kwa mara hasa kipindi cha majira ya mvua jambo ambalo hufanya baadhi ya wananchi kushindwa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa urahisi.
