Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
April 30, 2025, 1:34 pm

‘‘Naomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwefundisho kwa jamii kuacha tabia ya ukatili dhidi ya watoto’’. Aristariko Msongelo mwendesha mashitaka wa Jamhuri Wilaya ya Bunda.
Na Adolf Mwolo
Mahakama wilayani Bunda imemhukumu kifungo cha miezi 6 cha nje ya jela Neema Msimu John(28),Mkazi wa mtaa wa Mapinduzi kwa kosa la ukatali dhidi ya mtoto wake mwenye umri wa miaka minne kwa kumchoma moto kwenye mkono wake wa kushoto kwa kosa la kujisaidia hovyo.
Hukumu hiyo imetolewa Aprili 29, 2025 na Hakimu Mwandamizi,Betron Sokanya, baada ya mshitakiwa kukiri kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na kifungu C169A(1) na (2) cha kanuni ya adhabu ya sura ya 16 iliyofanyiwa marejeleo mwaka 2022.

Awali kabla ya hukumu kutolewa, mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri Aristariko Msongelo ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwefundisho kwa jamii kuacha tabia ya ukatili dhidi ya watoto.
Aidha Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Bunda Florence Debogo awewaasa wazazi kutotumia adhabu kali kwa watoto na badala yake watumie adhabu mbadala kama kumnyima mtoto kuangalia television na kuto kwenda kucheza ili kupunguza wimbi la ukatili kwa watoto.
Kwa upande mwingine baadhi ya wazazi na wananchi wilayani Bunda wamewashauri wazazi wenzao na jamii kwa ujumla kuacha kutoa adhabu kali kwa watoto ambazo zinapindukia na kuwa ukatili
