Bunda FM Radio

Wananchi wilayani Bunda wametakiwa kuchukua vitambulisho vyao vya Taifa (NIDA)

April 29, 2025, 12:22 pm

Kaimu Afisa Usajili wa Wilaya ya Bunda Hilkia Nyamongo akizungumza kwenye kipindi cha Busati la habari Bunda FM Radio. Picha na Amos Marwa.

Tumepokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa NIDA, James Kaji, kufikia mei mosi 2025 kuwa wananchi wote waliotumiwa ujumbe mfupi wa sms kujulishwa upatikanaji wa vitambulisho vyao lakini hawajajitokeza kuchukua vitasitishwa” Hilkia Nyamongo,kaimu Afisa usajili NIDA Wilaya ya Bunda.

Na Amos Marwa

Hayo yaamebainishwa na Kaimu Afisa usajili wa Wilaya ya Bunda, Hilkia Nyamongo wakati akizungumza na Bunda FM Radio kupitia kipindi cha Busati la habari.