Smile FM Radio

‘Wakulima zingatieni ushauri’

March 11, 2026, 9:29 am

Picha ya Afisa kilimo Halmashauri ya Babati Evatha Lyatuu akiwa ndani ya studio za Smile Fm

Wakati mkoa wa Manyara ukiwa katika kipindi cha masikia, wakulima wametakiwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo

Na Kudra Massaga

Wakulima wilaya ya Babati Mkoani Manyara wametakiwa kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wa kilimo pamoja na mamlaka ya hali ya hewa kabla ya kuanza kwa msimu husika ili kupata mavuno yenye tija.
Wito huo umetolewa na Afisa kilimo Halmashauri ya Babati Evatha Lyatuu wakati akizungumza kwenye kipindi cha Tunonge kinachorushwa na smile fm Radio.

Sauti ya Afisa kilimo Halmashauri ya Babati Evatha Lyatuu
Picha ya Afisa zana Halmashauri ya Babati Nathanael Pwele

Nae Afisa zana Halmashauri ya Babati Nathanael Pwele amesema kuwa saerikali kupitia wizara ya kilimo ipo katika hatua ya kwanza ya kuanzishwa kwa mradi wa vituo 1000 vya huduma ya zana za kilimo nchi nzima na Halmashauri ya Babati ikiwepo kwenye mpango huo.

Hata hivyo Pwele amewashauri wakulima kutumia zana bora za kilimo sio kwa kupata mazao yenye tija pekee bali pia ni kwa ajili ya kurahisisha kazi ya kuandaa mashamba pamoja na kilimo kinapoanza.