Smile FM Radio
Smile FM Radio
February 5, 2026, 12:39 pm

Picha ya meneja wa Benki ya NMB Baraka Ladislaus
Katika kuchangia wanafunzi kupata elimu bora na huduma bora za afya Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika zahanati na shule za msingi halmashauri ya Babati Mkoani Manyara
Na Linda Moseka
Benki ya NMB tawi la Babati imeendelea kujenga uhusiano mzuri na jamii kwani imefanikiwa kutoa misaada ya madawati na mabati katika shule za msingi na zahanati ndani ya halmshauri ya mji wa Babati.
Msaada umetolewa katika shule za msingi Singu B mabati 150, shule ya msingi Soraa mabati 155, shule ya msingi kiongozi madawati 50 na zahanati ya Imbilili zaidi ya mabati 134.
Kwa mujibu wa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Baraka Ladislaus amesema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono serikali nakujiweka karibu na jamii kwani ndio wanayofanya benki hiyo ipate mafanikio na kuwa benki bora ya maendeleo na pia ni vipaumbele vya taasisi kuhakikisha inaiunga mkono serikali na jamii kwa ujumla.
Sauti ya Meneja wa NMB kanda ya kaskazini Baraka Ladslaus
Aidha mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda na mgeni rasmi wa tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo, ameishukuru sana Benki ya NMB kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye jamii na namna wanavyoiunga mkono serikali kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo na kuifanya NMB kuendelea kuwa taasisi bora ya huduma za kibenki hapa nchini.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda
Baada ya msaada huo kutolewa na benki ya NMB afisa elimu msingi Saimon Mumbee amekiri kupokea madawati 50 na mabati 305 yatakayosaidia kuboresha miundombinu ya shule hasa mazingira bora ya kujifunzia na pia amewashukuru benki ya NMB kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika jamii
Sauti ya afisa elimu msingi Saimon Mumbee
Na kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kiongozi wameishukuru benki ya NMB kwa msaada huo wa madawati pamoja na mabati kwani yatasaidia kuboresha mazingira mazuri ya kusoma na kujifunza na pia kupata elimu bora.
Sauti ya wanafunzi