Smile FM Radio

Wananchi toeni ushahidi kesi za ukatili

May 6, 2025, 11:30 am

Mkaguzi msaidizi wa polisi Wilness kimario ambae pia ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto Mkoa wa Manyara. Picha na Mpiga picha wetu

Wananchi wanatakiwa kutoa taarifa za ukatiri kwenye mamlaka za serikali ili kukomesha matukio kama hayo kuendelea kujitokeza katika jamii

Na Mwandishi wetu

Jamii imetakiwa kutoishia kwenye kuripoti tu matukio ya kikatili bali wanatakiwa kujitokeza mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi ili wahalifu waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hayo yameelezwa na na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Wilness Kimario ambae ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Manyara wakati akizungumza na Smile Fm Radio.

Amesema changamoto kubwa inayojitokeza kwenye muendelezo wa kesi zinazoripotiwa ni kukosekana kwa ushahidi mahakamni jambo ambalo linarudisha nyuma hatua ya wahalifu kuchukuliwa hatua za kesheria.

Sauti ya mkuu wa dawati la jinsia na watoto

Licha ya Takwimu kuonyesha kuwa wahanga wakubwa wa matukio ya ukatili ni wanawake pamoja na watoto lakini kwa upande wa wanaume matukio ya ukatili yamekuwa yakijitokeza mara nyingi kwenye jamii hivyo A/INSP Kimario amesema jitihada kubwa ya kutoa elimu pamoja na kuijengea jamii uelewa kuhusu ukatili inafanyika, hivyo ni jukumu la kila mtu kupinga ukatili bila kujali jinsia yake.

Sauti ya mkuu wa dawati la jinsia na watoto

Ili kuhakikisha ukatili kwa watoto unakwisha kabisa Mkoani wa Manyara A/INSP Kimario amesema wameunda program ya madawati ya ulinzi na usalama kwa watoto wawapo shuleni na nje ya shule ili waweze kutolea taarifa za ukatili.

Sauti ya mkuu wa dawati la jinsia na watoto

.