About us

Radio Tadio ni jukwaa la usambazaji wa habari za kijamii zilizopo Tanzania.

Tambua

Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), hapo awali ikijulikana kama Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Kijamii Tanzania (COMNETA), ni mtandao wa kutengeneza na kuzalisha habari hasa zenye maudhui ya kijamii nchini Tanzania. TADIO imesajiliwa chini ya Sheria Nambari 24 ya mwaka 2002 ya usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na imepewa cheti namba 0009337.

Kwa sasa kuna redio 43 zinazozalisha vipindi vya kijamii na kurushwa nchi nzima (Tanzania bara na Tanzania visiwani).

Ofisi zetu zinapatikana makao makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam ambapo pia tuna studio zetu za uzalishaji wa vipindi.

Unakaribishwa sana na pia unaweza kuwasiliana nasi kushirikiana katika miradi mbalimbali yenye lengo la kuiwezesha jamii ya watu waliopo vijijini na Tanzania kwa ujumla.

Taarifa ni nguvu

RADIO TADIO tunaamini kuwa “Taarifa ni Nguvu” hivyo basi hatuna budi kuzalisha na kusambaza taarifa zenye viwango bora hasa kwa watu waliopo vijijini ili waweze kujihusisha moja kwa moja katika shughuli za maendeleo na kujitegemea.

  • Dira yetu: Jamii za vijijini ambazo zinapata na kutumia habari na taarifa za kweli na zenye uhakika kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
  • Dhima yetu: Kuwezesha watu wa vijijini kutumia habari za kweli na uhakika kwa maendeleo yao wenyewe.
  • Kauli mbiu: Fika wasikofika!