Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
October 6, 2025, 6:43 pm

Uongozi wa Butiama fm umewasisitiza waandishi wa habari kutoa habari zinazo zunguka jamii husika
Na Oscar Mwakipesile
Katika semina ya siku nne iliyoandaliwa na uongozi wa Butiama fm umewaasa waandishi wa habari kutoa taarifa za jamii husika ili kuwezesha wananchi wa jamii husika ya Butiama na Tarime kwa ujumla kusaidia kuinua jamii kupitia habari wanazoziandika ziwe zinalenga maeneo yanayozunguka mkoa wa tarime ili kutoa fursa kwa wananchi kufikiwa kwa urahisi kupitia vyombo vya habari wanavyo vifanyia kazi.

Semina hiyo ya kuwajengea uwezo wanahabari na kuwakumbusha juu ya kuandika habari za jamii yatafanyika kwa siku 4 katika ukumbi ulio katika makumbusho ya Baba wa Taifa J.K.Nyerere uliopo Mwitongo Butiama.
Aidha waandishi wamekumbushwa pia kutumia zaidi Lugha ya Taifa (Kiswahili) ilikuifikia jamii kwa urahisi na kueleweka kwa urahisi bila kuchanganya lugha.