Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
October 1, 2025, 2:13 pm

Tunatarajia kufungua Butiama FM katika ofisi zetu za Butiama zilizopo pale kwa Chifu Wanzagi kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.
Na Osiana Osca
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu uongozi wa Butiama FM unatangaza kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja kupitia masafa ya 91.3 fm siku ya tarehe tatu mwezi wa 10 mwaka 2025 .
Butiama FM inakukaribisha ewe mkazi wa Butiama pamoja na Mkoa mzima wa mara kukaribia kujumuika pamoja nasi kwenye ufunguzi wa radio hii ya Butiama Fm itakayofanyika katika ofisi za Butiama zilizopo pale kwa Chifu Wanzagi kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.
Tunakukaribisha sana ewe mwanabutiama kuandika historia pamoja ya radio yenu sauti ya jamii nguvu ya maendeleo.
