Zenj FM

Vikundi ni Njia ya Maendeleo kwa Jamii

6 October 2022, 1:34 pm

NA: Mary Julius na Thuwaiba Mohd : Mwakilishi wa jimbo la Paje Soud Nahodha Hassan wamewataka wakinamama kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kusaidiawa katika kujiletea maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Akizungumaza mara baada ya kuzindua na kukabidhi  kisima cha maji kwa kikundi cha furahia wanawake kilichojengwa kwa ufadhili wa banki ya biashara Tanzania,mwakilishi huyo amesema ni vyema wanawake wakajiunga na vikundi,kwani vikundi vimekuwa vikisaidia jamii na kuwa njia rahisi kwa wafadhili kuweza kuwafikia.

Aidha ameipongeza benki ya biashara Tanzania kwa kuwajali wateja wao kwa kurejesha faida kwa jamii na kutoa wito kwa bank nyingine kuiga mfano huo.

.

Akizungumaza mara baada ya kuzindua kisima cha maji Mkurugenzi mtendaji wa bank biashara Tanzania Sabasaba Mushingi  amesema kisima hicho kitawasaidia katika uzalishaji na kuokoa muda wa kufanya shughuli za maendeleo.

.

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi cha furahia wanawake  paje sihaba Mustafa ameishukuru banki hiyo kwa kuweza kutekeleza ahadi zake kwao na kusema Msaada huo utaweza kuongeza uzalishaji katika kiwanda chao cha kusanifu mwani.

.