Zenj FM

Mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA yapata ufumbuzi wa Tatizo la maji Zanzibar.

4 February 2022, 4:37 pm

Utiaji wa saini wa  utekelezaji wa miradi ya maji Zanzibar

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Dr Salha Mohammed Kassim amesema mamlaka ya maji zanzibar itahakikisha inajenga visima vya maji safi na salama katika maeneo yote ya unguja na pemba.

Akizungumza katika hafla ya utiaji wa saini wa  utekelezaji wa miradi ya maji kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa dhidi ya mapambano ya uviko 19 IMF katika ukumbi wa  hoteli ya serena Wilaya ya Mjini Unguja, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dr Salha Mohammed Kassim amesema Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar imekuwa  na jitihada ya kutumia mbinu mbali mbali  ili kuhakikisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi inafanikiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Dr Salha Mohammed Kassim

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Nishati Zanzibar Suleiman Masoud Makame amewataka wakandarasi waliopewa dhamana ya kutekeleza mpango huo kufanya haraka ili kuweza kuhakikisha azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuwapatia wananchi wake maji safi na salama inatimia.

Waziri wa Maji na Nishati Zanzibar Suleiman Masoud Makame

Akizungumza kwa niaba ya wakandarasi waliopewa dhamana ya kusimamia mpango huo Nassor Muhammed wameahidi kufanya kazi kwa mashirikiano na serikali ili kuweza kukamilisha azma hiyo kwa kufuata mikataba iliyosainiwa.

Mkandarasi Nassor Muhammed