Zenj FM

Kaskazini A Unguja na Micheweni Pemba, kunufaika na Pharm Acces

4 February 2022, 5:05 pm

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee na Watoto Nassor Ahmed  Mazrui akipokea vifaa vya afya.

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee na Watoto Nassor Ahmed  Mazrui amesema wizara ya afya itaendelea kushirikiana na mashirika binafsi  ili kuweza kuwasaidia wananchi wa visiwa vya Zanzibar.

Akizungumza katika makabidhiano ya  kupokea vifaa vya kuboresha huduma za afya kwa mama wajawazito na watoto Waziri Mazrui  amelipongeza   shirika la Pharma Acces kwa kuuona uhitaji wa vifaa tiba katika Wilaya mbili ya Kaskazini Unguja  na Micheweni Pemba.

Sauti: Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee na Watoto Nassor Ahmed  Mazrui

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi  wa Shirika la  Phama Acces Tanzania Dk Kheri Marwa amesema Pharm Acces imejikita katika kuboresha huduma za afya ya  mama na mtoto.

Sauti: Mkurugenzi Mkaazi  wa Shirika la  Phama Acces Tanzania Dk Kheri Marwa

Shirika la Pharma Acces limetowa vifaa vyenye thamani ya million 92 kwa wizara ya afya ustawi wa jamii wazee na watoto  kwa lengo la kuboresha huduma hizo.