Zenj FM

Pharm Access waleta neema Zanzibar

2 December 2021, 2:51 pm

Na Fatma Ali Mohd:Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee  na Watoto Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikishirikiana na Shirika lisilo la kiserikali Pharm Access linaandaa mikakati ya kuhakikisha Zanzibar inaanzisha mfuko wake  wa huduma za afya.

Akizungumza katika  mkutano na shirika hilo kwenye ukumbi wa Golden Tulip Mazrui amesema mchakato huo ukikamilika utaweza kutoa fursa kwa wananchi wote kupata huduma bora za afya kwa uhakika.

Sauti ya Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Safe Care Dr Peter Risha amesema lengo la taasisi hiyo kuja Zanzibar ni kuandaa mchakato wa kuazisha bima ya afya ili kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kutokana na kuongezeka kwa harama za afya, taasisi hiyo itashirikiana  na Wizara ya Afya Zanzibar na kuhakikisha inatafuta mbinu ili  kila mwananchi apate na kufikiwa na huduma za afya zilizobora.

Sauti ya Mkurugenzi wa Safe Care Dr Peter Risha