Zenj FM

Madereva wa daladala watakiwa kutoingia na abiria sheli

24 November 2021, 1:26 pm

Na Thuwaiba Mohd: Afisa  uhusiano wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nisharti Zanzibar ZURA Hassan Juma Amour amewataka wasimamizi wa vituo vya  mafuta sheli kutoruhusu mtowa huduma kujaza mafuta kwenye gari ikiwa na abiria ili kuepusha  athari zinazoweza kujitokeza.

Akizungumza na zenj fm katika ofisini za zura  maisara mjini unguja afisa Hassan amesema kwa mujibu wa sheria za vituo vya mafuta  ni kosa gari kujazwa mafuta ikiwa na abiria.

Nae muhasibu wa kituo cha kijangwani petrol station Abdallah rajab haji amesema ni vyema wahudumu wa sheli kutojaza mafuta kwa gari ambayo itakuwa na abiria.