Uyui FM Radio

Maagizo matano kwa wakuu wa wilaya Tabora

3 February 2023, 3:16 pm

Mkuu wa mkoa wa TABORA Balozi Daktari Batilda Buriani ametoa maagizo matano kwa Wakuu wa wilaya wa mkoa huo likiwemo la kwenda kusimamia masuala ya ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Maagizo hayo ameyatoa kwenye hafla ya uapisho wa wakuu wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi uliopo  ofisi ya mkuu wa mkoa.

Daktari Batilda akimuapisha mkuu wa wilaya ya Nzega
Sauti ya mkuu wa mkoa

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa, ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhan Kapela amewaasa Wakuu wa wilaya wapya kuwa wasikivu na watenda haki katika majukumu yao.

Sauti ya Mstahiki Meya

Nao Wakuu wa wilaya wapya  Zakaria Mwansasu wa wilaya ya Uyui na Naitapwaki Tukai wa wilaya ya Nzega wameahidi kwenda kutekeleza maelekezo.

Sauti za wakuu wa wilaya wa Nzega na Uyui