Uyui FM Radio

Waandishi wahimizwa kusaidia jamii kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi

12 December 2021, 7:34 pm

Waandishi wa habari wamehimizwa kuandika na kutangaza habari kuhusu utunzaji mazingira ili kusaidia jamii na dunia kwa ujumla kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yameelezwa katika mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika habari za mazingira nchini Tanzania yaliyofanyika mkoani Katavi.

Mratibu wa mafunzo hayo Prosper Kwigize  amesema waandishi wengi wa habari nchini hawajawekeza nguvu vya kutosha kwenye kuripoti habari za mazingira kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo waandishi wengi kukosa ubobezi katika masuala ya mazingira

Kwigize amehimiza waandishi wa habari kujikita katika kutoa elimu ya mazingira na uhifadhi kwa kushirikisha wananchi ili kuibua changamoto na kuzipatia ufumbuzi utakao saidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

waandishi
sauti ya KWIGIZE.

Baadhi ya waandishi walioshiriki mafunzo hayo wameahidi kufanyia kazi ujuzi walioupata katika kusaidia jamii na taifa kwa ujumla kuepukana na athari za mabadiliko ya tabia nchi

INSERT: WAANDISHI WA HABARI

sauti za waandishi wa habari

Pamoja na mambo mengine washiriki wamesisitiza uwepo wa juhudi ya pamoja kati ya mamlaka za uhifadhi,serikali,wanasiasa na vyombo vya habari katika kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa jamii ili kutatua tatizo la uvamizi na uharibufu wa mazingira kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo