Uyui FM Radio

Mwanamke atajwa kuwa mhanga wa mabadiliko ya Tabia ya nchi

12 December 2021, 7:46 pm

Wanawake wamehimizwa kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa ni wahanga wakuu wa athari za mabadiliko ya tabia nchi katika jamii

Katibu mtendaji  wa taasisi ya OHIDE Silesi Mali Mali amesema wanawake wamekuwa nguzo katika uendeshaji wa familia na wengi  hutegemea kilimo na ujasiriamali hivyo mabadiliko ya tabia nchi huathiri shughuli zao moja kwa moja

OHIDE Silesi Mali Mali
sauti ya OHIDE Silesi Mali Mali

Beatrice Venance kutoka shirika la Good Harvest ametoa wito kwa wanawake na jamii kwa ujumla kuendelea kutunza mazingira pamoja na kuendelea kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Sauti ya Beatrice Venance

Wakati huohuo mkurugenzi wa shirika la Good Harvest Filbert Chundu amesema wanaendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kuanzia mashuleni na kupitia michezo ambayo inaambatana na upandaji miti

INSERT: FILBERT CHUNDU

Sauti ya Filbert Chundu

Hayo yanajili wakati ambapo Tanzania na nchi nyingi duniani zikikabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaathiri upatikanaji wa mvua,shughuli za kilimo na uzalishaji hali inayotishia ukosefu wa chakula na kudolola kwa uchumi duniani