Uyui FM Radio

Katibu Hospitali ya Rufaa Kitete kufanyiwa uchunguzi wa kinidhamu

20 April 2021, 5:41 pm

Watumishi wa afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora -Kitete wamemuomba mkuu wa mkoa wa Tabora kufanya uchunguzi wa kinidhamu dhidi ya Katibu wa Hospitali hiyo BABY NYIMBO kutokana na tuhuma mbalimbali za kiutendaji.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wengine wa Hospitali hiyo afisa muunguzi ADELINA ILOGOLA  amesema katibu huyo amekuwa ni kero kutokana na kutozingatia misingi ya utumishi.

Bi Adelna Ilogola 
Sauti ya Adelina Ilogola

Kufuatia malalamijko hayo mkuu wa Mkoa wa Tabora Doktari PHILLEMON SENGATI ametoa maagizo katika ofisi ya katibu tawala wa Mkoa kufanya uchunguzi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi wa hospitali hiyo.

Dkt. Philemon Sengati
Sauti ya Dkt.Sengati

Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa amesisitiza utendaji wenye maadili ya taaluma hiyo kwa kufuata misingi ya utumishi bora.

Sauti ya Dkt.Sengati

Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Tabora Dokta PHILLEMO SENGATI kufanya ziara katika hospitali hiyo kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo.