Uyui FM Radio

Malalamiko 50 kati ya 116 yakutwa na viashiria vya rushwa -TABORA.

15 April 2021, 6:09 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Tabora  imepokea jumla ya malalamiko 116 ambayo kati yake 50 yalikuwa na viashiria vya rushwa.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari   naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora  Mashauri Elisante amesema katika uchunguzi wa mashtaka  kwa kipindi cha mwezi January  hadi march mwaka huu  pia wamefungua kesi tano mahakamani.

Waandishi wa habari pamoja na Naibu mkuu wa TAKUKURU- TABORA Mashauri Elisante.
Sauti ya naibu mkuu wa TAKUKURU- TABORA Mashauri Elisante.

Katika hatua nyingine Elisante amebainisha kuwa  katika kipindi hicho  TAKUKURU mkoa wa Tabora imefanya  uchambuzi  katika mfumo wa utoaji wa vibali vya ujenzi  ndani ya halmashauri  zote za mkao wa Tabora  ambapo pia imefuatilia  utekelezaji  ya miradi ya maendeleo katika maneo mbalimbali.