Uyui FM Radio

Milioni 18 kugharamia ujenzi matundu ya vyoo 13 S/M GONGONI.

8 April 2021, 5:25 pm

Zaidi ya shilingi milioni 18 zimegharamia ujenzi wa matundu ya vyoo 13 katika shule ya msingi GONGONI kata ya KANYENYE Manispaa ya TABORA.

Mhashamu Askofu Mkuu jimbo katoliki TABORA PAUL RUZOKA amesema hayo wakati wa kukabidhi jengo lenye matundu 13 ya vyoo na kusema kwamba uamuzi wa kujenga umekuja baada ya kuona adha wanayoipata wanafunzi shuleni hapo.

Mhashamu Askofu mkuu jimbo kuu Katoliki TABORA PAUL RUZOKA.
sauti ya Mhashamu Askofu PAUL RUZOKA

Akitoa Shukurani kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispaa ya TABORA ,Afisa elimu msingi JOEL MKUCHIKA amesema ujenzi wa matundu hayo ya vyoo utachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mahudhurio ya wanafunzi shuleni.

Sauti ya Afisa elimu msingi Joel Mkuchika

Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi GONGONI FREDY MWIGA ameahidi kusimamia vyoo hivyo kwa kuhakikisha vinatuzwa na kudumu kwa muda mrefu.

Sauti ya mkuu wa shule ya GONGONI Fredy Mwiga

Jengo hilo ambalo limejengwa na fedha kutoka chini ya kanisa Katoliki jimbo kuu TABORA linaidadi ya matundu ya vyoo 11 vya wanafunzi na viwili (2) vya walimu.