Uyui FM

Someni mapato na matumizi ni takwa kisheria-DC Tabora

23 August 2021, 19:50

Mkuu wa wilaya ya TABORA Dkt YAHAYA NAWANDA amemuagiza mtendaji wa kata Ya Isevya GATI ADAMU ahakikishe anasimamia suala la usomaji wa mapato na matumizi kwa wananchi kwenye kila mtaa, kisha kupeleka ripoti hiyo ofisini kwake hadi kufikia ijumaa ya wiki ijayo.

Akizungumza katika ziara yake kwenye kata hito Dkt NAWANDA amesema suala la usomaji wa mapato na matumizi kwa wananchi ni wajibu wa watendaji wa mitaa pamoja na kata husika.

Dkt Nawanda
Sauti ya Dc Nawanda

Kwa upande wake mtendaji wa kata hiyo GATI ADAMU amesema atahakikisha anasimamia na kufuata maagizo yote aliyopewa na mkuu wa wilaya kwa wakati.

Mtendaji Gati
Sauti ya mtendaji wa Isevya

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya TABORA Dkt NAWANDA amewasisitiza viongozi wa mitaa, kuacha kukaa ofisini na badala yake waatue migogoro ya wananchi ambayo inaweza kurudisha nyuma maendeleo.