Uvinza Fm

“Wafanyabiashara wa Mafuta ya mawese zingatieni matumizi sahihi ya vipimo”

05/05/2023, 11:57 am

Na glory Kusaga

Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma hususani wauzaji wa Mafuta ya mawese wameaswa kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo na kuacha kutumia kipimo cha bidoo kwani siyo kipimo sahihi na kinafanya Serikali kushindwa kukusanya kodi kwa usahihi na kufanya maisha wauzaji wa bidhaa hiyo kushindwa kujikwamua kiuchumi

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwenye kikao cha kujadili mikakati ya namna ya kutokomeza vipimo batiri vinavyotumika kuuzia Mafuta ya mawese maarufu kwa jina la bidoo ndani ya Mkoa wa Kigoma .

Sauti mkuu wa wilaya Buhigwe

Kwa Upande wake Meneja wa wakala wa Vipimo Mkoa wa Kigoma Laulenti Kabikiye amesema wamekuwa wakitoa elimu juu ya matumizi ya kipimo hicho cha bidoo nakuwa tathimini ya awali inaonyesha matumizi ya kipimo hicho yameanza kupungua ndani ya Mkoa wa Kigoma.

Sauti ya Meneja wa Vipimo

Kwa Upande wao baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki kwenye kikao hicho akiwemo Meneja wa shirika la viwango Tanzania Mkoa wa Kigoma Rodney alananga wamesema ili kuhakikisha wauzaji wanatumia Vipimo hivyo iwepo bei rafiki ya kununua Vipimo hivyo nakuwa Mafuta ya mawese inatakiwa yapewe nembo ya ubora ili kuyatangaza Mafuta ya mawese.

Sauti wafanyabiashara

Hata hivyo kikao hicho kimeweka baadhi ya maadhimio  ikiwemo kuwepo kwa  vituo Maalumu  vya kuuzia bidhaa ya mawese ili kuweka urahisi wa kudhibiti wauzaji ambao wamekuwa hawazingatii Vipimo sahihi, kuweka bei rafiki ya kununua Vipimo hivyo hivyo kutoka zaidi ya Shilingi Laki Moja hadi Shilingi elf 90 na kutunga sheria ndogo kwa ajili ya kusimamia uuzaji wa bidhaa ya mawase