Uvinza Fm

Mikutano ya kisheria husaidia kutatua migogoro ya wananchi

12/01/2022, 7:01 pm

Na,Rosemary Bundala

Mikutano ya kisheria katika halmashauri za vijiji imetajwa kuwa njia mojawapo ya kutatua matatizo pamoja na migogoro  kwa wananchi

Hayo yamezungumzwa na wanachi wa wilaya ya uvinza mkoani Kigoma Bwana VICENT LAZARO na  Bi MWAMINI JUMA  wakati wakizungumza na redio uvinza fm ambapo wamesema mikutano ya kisheria husaidia pale panapokuwa na migogoro na matatizo ya kijiji

Sauti za wananchi

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kibaoni wilayani uvinza bwana  MUSSA RAMADHANI  amesema mikutano ya kijiji husaidia japo mwitikio hua mdogo kutoka  kwa wananchi na akatoa ushauri kwa kwa wananchi katika kuhakikisha wanajitokeza kushiriki katika mikutano ya kijiji

Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji

Nae mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha ruchugi wilayani uvinza mkoani kigoma bwana RAMADHANI SAID KAYUNGILO  ameelezea maana ya mikutano ya kisheria pamoja na umuhimu wa mikutano hiyo

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji

Mikutano ya kisheria katika ngazi za vijiji bado inaonekana kuwa chanzo bora cha wananchi kusemea matatizo na shida za kijiji kwa urahisi katika maeneo yote nchini.