Uvinza Fm

Mabomba ya maji yenye thamani ya shilingi milioni 600 yatolewa na serikali

24/11/2021, 3:59 pm

Na,Glory Paschal

Mabomba ya Maji yenye thamani ya Shilingi milioni 600 yametolewa na Serikali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambayo yanaanza kutandikwa katika kata kadhaa ikiwemo kata ya Bangwe

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. ESTER MAHAWE  amesema hatua  hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya kutimiza adhima ya kumtua ndoo Mama kichwani ifikapo mwaka 2025 kwa kuhakikisha huduma ya maji inafika maeneo yote

Sauti ya mkuu wa wilaya kigoma mjini

Naye Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira KUWASA, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhandisi JONAS MBIKE, amesema wamejipanga kuhakikisha wanafikisha huduma ya maji kwa wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hiyo, huku akitaja maeneo ambayo mabomba hayo yatatandikwa

Sauti ya meneja kuwasa

Baadhi ya wananchi Kata ya Bangwe, ambao ni miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na utandikaji wa mabomba hayo, wameiomba KUWASA kuanza zoezi hilo mapema, ili waondokane na adhaa inayowakabili ya kutopata maji safi na salama.

Sauti za wananchi