Uvinza Fm

Serikali mbioni kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana

07/10/2021, 5:53 pm

Na,Glory Paschal

Waziri wa Nishati JANUARY MAKAMBA amesema serikali iko katika mchakato wa kuhakikisha inafikisha umeme wauhakika Mkoani Kigoma kwa kuunganisha Mkoa huu na Gridi ya Taifa kutoka vituo vya Nyakanazi na Tabora

Mh. MAKAMBA  amesema hayo wakati alipotembelea Kituo cha Kuzalisha umeme cha Bangwe na Kasulu ili kujionea hali ya uzalishaji wa umeme kwa mkoa wa kigoma kufutia tatizo la umeme kukatika mara kwa mara Mkoani hapa

Sauti ya waziri wa nishati

Naye Mkurugenzi wa Tanesco Nchini MAHARAGE CHANDE  hatua zimeshaanza kuchukuliwa kwa kupunguza baadhi ya njia za umeme zilizokuwa zinategemea umeme na kuwa wameongeza uzalishaji wa mega wat 8.75 ili kuongezza nguvu ya upatikanaji wa umeme

Sauti ya mkurugenzi Tanesco nchini

Katika hatua nyingine akiwa wilayani Kasulu Waziri Makamba amesema serikali imetoa shilingi bilioni moja kati ya bilioni sita zinazohitajika ili kuongeza upatikanaji wa umeme katika mji wa kasulu ambao mitaa 76 haina umeme kwa sasa.