Uvinza Fm

Majambazi watatu wauawa

29/09/2021, 6:34 pm

Na,Glory Paschal

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika barabara inayotokea  kijiji cha Kagerankanda kata ya Nyakitonto Tarafa ya Buhoro wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi Kasmishina msaidizi wa Jeshi la Polisi  mkoa wa Kigoma ACP JAMES MANYAMA  amesema tukio hilo limetokea September 28 mwaka huu.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi Kigoma

Aidha Kamanda MANYAMA ameongeza kuwa miongoni mwa majambazi ho watatu wametoroka huku Jeshi hilo limefanikiwa kukamata Bunduki aina ya AK 47 pamoja na mapanga mawili yaliyokuwa yakitumiwa na majambazi hao.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi kigoma

Katika Hatua nyingine kamanda MANYAMA  amesema juhudi za kuwasaka majambazi hao watatu waliotoroka zinaendelea huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi kigoma

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa uhifadhi, Hifadhi ya Gombe YUSTIN NJAMASI  amesema kuwa jukumu lao ni kuzuia matukio kabla hayajatekelezwa na komba ushirikiano baina yao na wananchi uendelezwe.

Sauti ya muhifadhi ,hifadhi ya Gombe