Uvinza Fm

Utalii waongezeka hifadhi ya Ruaha baada ya kupungua kwa covid 19

09/09/2021, 5:44 pm

Na,Glory Paschal

Imeelezwa kuwa katika Kipindi cha Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona awamu ya kwanza na ya pili hali ya watalii kutembelea hifadhi za Taifa Ikiwemo Ruaha ilipungua ikilinganishwa na wakati huu ambapo watalii wameanza kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi hiyo

Hayo yamebainishwa na Afisa Uhifadhi Kitengo cha Utalii  AHMED NASSORO Kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha alipotembelewa na waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa tofauti hapa Tanzania, ambapo amesema  kwasasa watalii wameongezeka kwani wageni 500 hadi elfu 5000 kwa mwezi hutembelea hifadhi hiyo

Sauti ya afisa uhifadhi Ruaha

HALIMA KIWANGO mhifadhi kitendo cha Ekolojia katika Hifadhi ya Taifa Ruaha amesema changamoto  kubwa katika hifadhi hiyo imekua ni kukauka kwa  maji kwenye mto  hasa nyakati za kiangazi hali inayopelekea  kupoteza uasilia wa hifadhi hiyo pamoja na wanyama hivyo kuwaomba wananchi waliopo pembezoni kulinda vyanzo vya maji huku hifadhi ikiendelea na juhudi ya kuhakikisha wanaunusuru mto huo

Sauti ya mhifadhi Ekolojia Ruaha

Nae mratibu wa waandishi wahabari wanawake Tanzania bi MARY MWAKIBETE na wadau wengine wa utalii wamesema juhudi za kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa vivutio vya utalii na kuwekeza sehemu mbalimbali itasaidia  kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla na watu kujitokeza kutalii katika vivutio mbali mbali

Sauti ya mratibu wa wanahabari wanawake

Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ilianzishwa Mwaka 1910 ikiitwa Saba Game Reserve na baada ya kuboreshwa na kuongezewa maeneo kuwa na uwezo wa kuhifadhi Tambo ilibadilishwa jina mwaka 1964 na kusajiliwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha ikiwa na ukubwa Kilomita elfu 20,226 na kuifanya hifadhi hiyo kuwa ya pili kwa ukubwa Tanzania.