Uvinza Fm

Kuwahi mapema kliniki kwa mama mjamzito husaidia kiafya

09/09/2021, 5:54 pm

Na,Editha Edward

Imeelezwa kuwa kuwahi mapema kliniki kwa mama mjamzito humsaidia kujua hali ya mama kiafya Pamoja na hali ya  mtoto wake aliyeko tumboni

Akizungumza na redio Uvinza fm mganga mkuu wilaya ya Uvinza dkt ZAITUNI HAMZA amesema kuna baadhi ya akina mama ambao hupuuzia kwenda kliniki pale wanapojitambua ni wajawazito kitendo ambacho hakikubaliki kiafya

Sauti ya mganga mkuu Uvinza

Dkt ZAITUN ameongeza kuwa kwa sasa serikali imeweka mkakati wa kumfatilia kila mama mmoja mmoja kwenye kila Kijiji ili kubainisha mama ambaye ana ujauzito na hajafika kliniki ili aanze kwenda lengo likiwa ni kumvusha salama mama mjamzito hadi pale atakapojifungua

Sauti ya mganga mkuu uvinza

Baadhi ya akina mama wilayani hapa wameeleza faida za kwenda kliniki mapema

Sauti ya mama

Hata hivyo Shirika la afya duniani WHO linashauri mama kwenda kliniki kuanzia mara nne katika kipindi chote cha ujauzito ili kufanyiwa vipimo na matibabu ya afya ya mama na mtoto kwa ujumla.