Uvinza Fm

Apoteza maisha kwa kukatwa na kitu kikali shingoni

02/09/2021, 5:51 pm

Na,Jacob Kapaya

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JACKIAS KIPARA mkazi wa kijiji cha Ruchugi wilayani Uvinza mkoani Kigoma  mwenye umri wa miaka 31 amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni.

Kamanda wa jeshi  la polisi mkoa wa kigoma JAMES MANYAMA  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na hapa analizungumzia

Katika hatua nyingine  kamanda MANYAMA  amewashukuru wananchi na kuwahimiza kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa

Sauti ya kamanda wa polisi kigoma

Mwenyekiti wa kijiji cha Ruchugi Ramadhan Said  amekiri kupokea taarifa ya kifo hicho  huku akiweka wazi aina  ya matukio ambayo yamewahi  kujitokeza ndani ya kijiji hicho.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji

Redio uvinza FM imepata nafasi ya kuzungumza na ndugu wa karibu wa marehemu ambae ni LUCAS  KIPARA  amesema kuwa mpaka kifo kinamkuta kijana   huyo hakuwa katika mazingira ya Nyumbani.

Sauti ya ndugu wa marehemu

Ikumbukwe kuwa marehemu ameacha mke pamoja na watoto 5 ambapo kati ya hao watoto wawili wanasoma shule darasa la kwanza na watoto 3 hawajaanza shule