Uvinza Fm

Wafanyabiashara wa vyombo vya moto waiomba serikali kushusha bei ya mafuta

13/08/2021, 7:31 pm

Na,Rosemary Bundala

Wafanyabiashara wa vyombo vya moto vya usafiri kutika kijiji cha Ruchugi wilayani uvinza mkoani kigoma wameiomba serikali kuwa tatulia suala la kupanda kwa bei ya mafuta  kutokana na hali ya kiuchumi ilivyo kwasasa.

Wakizungumza na redio uvinza fm wafanya biashara hao wamesema kuwa hali kwa sasa sio nzuri kiuchumi hivyo wanaiomba serikali iweze kupunguza bei hiyo ili iwasaidie kupata pesa ya ya kujikimu  na maisha ambapo mafuta hayo kwasasa yamepanda kutoka 2,400 hadi kufikia 2,700.

  

sauti za wafanyabiashara

Nae Raphael Mgaya ambae ni katibu mtendaji wa  Tanzania  Association  of oil  Marketing Companies (Taomac) amaelezea sababu zilizopelekea mafuta hayo ya petrol kupanda bei.

                       

Sauti ya katibu mtendaji

Kupanda kwa mafuta ya petrol  ni agizo lililotolewa na  Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) ambapo ilitangaza bei kikomo za bidhaa ya mafuta ya petrol hapa nchini ambapo zilianza julai 1 mwaka huu ikiwa ni kuendana na sheria ya fedha ya mwaka 2021.